Timu yetu ina miaka 81 lakini hatuna hata uwanja – MO Dewji (+Video)
Baada ya kutangazwa kwa Mfanyabiashara, Mohammed Dewji kushinda zabuni ya kuindesha klabu ya Simba kwa kumiliki hisa asilimia 49 ya timu hiyo, MO amesema anashangazwa klabu hiyo kukosa hata uwanja wa mazoezi licha ya kuwa na jina kubwa barani Afrika. “Leo hii timu yetu ina miaka 81 lakini hatuna hata uwanja wetu wenyewe wa kufanyia mazoezi. “amesema MO Dewji na kudai na kuahidi kujenga uwanja wa kisasa wa mazoezi wa klabu hiyo. Msikilize hapa chini akifunguka zaidi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa zabuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni